Jumanne , 9th Apr , 2024

Rapa na Producer J Cole ameomba radhi mbele ya mashabiki zake kupitia tamasha lake la ‘Dreamville Fest’ kwa kujibu disstrack ya Kendrick Lamar kupitia ngoma yake ya “7 Minute Drill” inayopatikana kwenye Album yake mpya ya Might Delete Later.

Picha ya J Cole na Kendrick Lamar

J Cole amekiri kuwa kurekodi wimbo wa kumdiss Kendrick Lamar ni jambo baya zaidi kuwahi kulifanya katika maisha yake na ngoma hiyo ataitoa kwenye Platform zote za kustream muziki.

Bifu la wawili hao limeibuka baada ya Kendrick Lamar kumdiss J Cole na Drake kwenye ngoma ya ‘I like that’ collabo aliyofanya na Future, Metro Boomin.