
Izzo Business
Kutokana pia na tafsiri tofauti, akitazamwa na wengine kama mpotoshaji jamii kwa ujumbe wa matamanio kwa mashemeji, Izzo amelazimika kufafanua kuwa rekodi yenyewe unahusisha tu hisia za kukubali shemeji alivyokaa sawa, na hii ni bila kuvuka mipaka yoyote.
Izzo ameeleza kuwa, hisia za namna hiyo zimekuwa ni kitu cha kawaida katika maisha ya kila siku, ingawa kwa namna yoyote ile ahamasishi kitendo cha watu kuchukua hatua za kufanya mapinduzi katika mahusiano ya ndugu na marafiki zao, kauli ambayo inaweka sawa wale wote ambao walikuwa wanamuelewa tofauti katika hilo.
Kuhusiana na baadhi ya watu kuona kuwa bado rekodi hiyo haijafikia kiwango kutokana na ukubwa na ubora wa wasanii aliowashirikisha G Nako pamoja na Mwana FA, na pia Producer Nahreel, hii ndio kauli ya Izzo, exclusively kupitia eNewz, ambapo ameeleza kuwa anachukulia kama moja ya changamoto ya kuendelea kufanya vizuri zaidi, akiamini kuwa hakuna kitu ambacho binadamu anaweza kukifanya kikakubaliwa na watu wote kwa asilimia 100.
Kwa maelezo yake binafsi, unaweza kumsikiliza Izzo Business hapa;
