Jumatatu , 7th Nov , 2022

Msanii wa HipHop Izzo Bizness ameshea taarifa ya kumpoteza shangazi yake kwenye ajali ya  ndege ya abiria kampuni ya 'Precision Air' kuanguka ndani ya Ziwa Victoria Bukoba mkoani Kagera. 

Izzo Bizness ameshea ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa Twitter akiandika "Shangazi yangu amefariki kwenye ajali ya ndege iliyotokea leo". 

Ndege hiyo ilikuwa na jumla ya watu 45 japo taarifa ya awali ilisema ina watu 43 , miili iliyopatikana 19 na waliookolewa ni watu 26.