Jumamosi , 12th Apr , 2014

Baada ya mahusiano ya mwanadada Zari na baba watoto wake Ivan Ssemwanga kuvunjika hivi karibuni na Zari kuonekana akiwa katika mahusiano mapya na mwanaume ambaye amefahamika kwa jina la Farouk, Ivan ameamua kuvunja ukimya kuhusu kuachana kwao.

Ivan Zari na watoto wao

Ivan katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni amesema kuwa, Zari kwa sasa ameyumba kifedha tofauti na yeye ambaye hutengeneza mamilioni ya shilingi kila mwezi, na mwanaume ambaye Zari anatoka naye sasa, alikuwa mlinzi huko Uingereza huku akisisitiza kuwa kati yake na Zari hakuna swala la talaka kutokana na wao kutokuwa na mkataba rasmi wa ndoa.

Zari pamoja na Ivan ambao wana watoto watatu pamoja, wamekuwa na historia ya kugombana na kutengana mara kwa mara, na safari hii mpasuko katika mahusiano yao umeonekana kuwa mkubwa kiasi cha kuua matumaini ya wawili hawa kurudisha mapenzi yao tena.