Jumatano , 25th Mar , 2015

Msanii wa muziki wa miondoko ya Jazz nchini Uganda, Isaiah Katumwa anatarajia kusherehekea maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanza kwake muziki huko Jijini Kampala, tukio litakalofanyika terehe 8 mwezi Mei mwaka huu.

msanii maarufu wa muziki wa Jazz nchini Uganda Isaiah Katumwa

Katika tukio hilo, Katumwa amejipanga kuliongezea ladha zaidi kwa kumualika msanii mkongwe Hugh Ramopolo Masekela kutoka Afrika Kusini, ambaye naye pia atapafomu Live katika tukio hilo la kihistoria.

Staa huyo anajivunia kushikilia kile anachokifanya akiendelea kuimarika kiuwezo kila siku, tangu mwaka 1995 ambapo ndipo alipoanza kufanya rasmi kazi hiyo.