Ijumaa , 5th Dec , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Iryn Namubiru amekuwa moja kati ya watu ambao wamefanikiwa kuhitimu masomo ya chuo kikuu, ambapo ametunukiwa shahada katika fani ya Utalii na Usimamizi wa Hoteli.

Msanii wa muziki wa nchini Uganda Iryn Namubiru

Sherehe ya kutunikiwa shahada kwa msanii huyu inafanyika leo nchini Uganda katika Chuo Kikuu cha Cavendish wakati ambapo msanii huyu yupo huko Uingereza kwa shughuli zake za kimuziki.

Hatua hii ambayo amepiga Iryn imeelezwa na wadau kuwa mfano wa kuigwa kwa mabinti nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla kutokana na umuhimu wa swala zima la Elimu katika dunia ya sasa.