Jumatano , 4th Mar , 2020

Msanii wa filamu na muziki Hemedy PHD, amefunguka na kusema yeye na malkia wa BongoMovie Irene Uwoya ni watu wa karibu sana, ambao wanatabia ya kupeana pesa pale mmoja wapo anapohitaji msaada.

Hemedy Suleiman na Irene Uwoya

Hemedy PHD amesema Irene Uwoya ni sehemu ya familia yake kwa sababu, wamekuwa wakisaidiana kuanzia ushauri, bata na kazi na mara ya mwisho alipewa Shilingi milioni moja na laki saba.

"Irene Uwoya ni mwanangu tunasaidiana vitu vingi sana vya kimaisha, hata nikimwambia nimekwama atanilinda kuanzia ushauri, pesa, bata na kazi kwahiyo tupo karibu na kwangu ni zaidi ya familia, mara ya mwisho ilikuwa mwezi wa 6 mwishoni nilimpigia simu akanipa kama moja ya saba hivi" amesema Hemedy PHD.

Mengine zaidi tazama kwenye video hapo chini.