Ijumaa , 31st Oct , 2014

Staa mwenye mvuto mkubwa hapa Bongo, Wema Sepetu aka Mamaa Dangote amewataka mashabiki wake kukaa tayari na ujio mpya wa kipindi chake cha uhalisia cha In My Shoes kuanzia wiki ijayo, kupitia hapa hapa Ting'a Namba Moja la Vijana EATV.

Wema Sepetu

Wema Sepetu ambaye wengi wamekuwa wakitamani kuona kile kinachoendelea katika maisha yake, anatoa nafasi hii kwa mara nyingine akiwa amejipanga zaidi kuleta burudani ya aina yake, nahapa anazungumzia ujio mpya wa In My Shoes ukiwa na mpenzi wake mwenye mapichapicha mengi, Diamond Platnumz.

Wema amesema kuwa, show hii itaanza kuruka siku ya Ijumaa tarehe 07 mwezi wa 11 kuwaonesha watu Msimu mpya uliojaa mvuto na burudani ya aina yake kwa wapenzi wa staa huyu.