Jumatano , 4th Mar , 2020

Mchekeshaji Idris Sultan ametoa barua ya maombi ya imani kwa kuomba watu wamuamini na apewe nafasi, katika kulisukuma gurudumu la tasnia ya filamu hapa nchini.

Picha ya mchekeshaji Idris Sultan

Akitoa taarifa hiyo kupitia mitandao yake ya kijamii ya Twitter na Instagram, Idris ametaka watu kumsapoti kwa kuingia mtaani kutafuta vipaji na kuwatengenezea vijana njia.

"Ndugu zangu movies sio kama mziki, kwamba utaitwa stage ukaigize series yako ulipwe au utapiga tour unaigiza kwenye majukwaa, kuna vipaji vingi sana mtaani ninavyojaribu kuvitengenezea njia, inaweza kuwa wewe au hata mtoto wako" ameandika.

"Ninachowaomba ni mniamini na mnipe nafasi nisukume hili gurudumu kwa ajili ya familia zaidi ya milioni ninazozijua, zitategemea kwenye hii njia ninayotengeneza, ahsante kwa upendo wenu na sapoti yenu" ameongeza.