Alhamisi , 13th Aug , 2015

Msanii chipukizi wa miondoko ya Bongofleva mzaliwa wa Mbeya mwenye maskani yake mkoani Morogoro Ice One ameelezea kuwa mchakato wa vijana kujiandikisha kupiga kura ulichukua sura mpya baada ya wasanii wa muziki na waigizaji kujitokeza.

msanii wa bongofleva kutoka mkoani Mororgoro Ice One

Ice One ambaye hivi sasa ametoa video yake mpya ya 'Niwe Nawe' ameongea na eNewz kuhusiana na hatua ya wasanii mbalimmbali akiwemo Profesa Jay ambaye hivi sasa ameshinda katika kura za maoni katika jimbo la Mikumi mkoani Mkoani Morogoro ili kuwania Ubunge kwa tiketi ya chama cha Demokrasia (CHADEMA).