Jumamosi , 31st Jul , 2021

Rapa na mwanamitindo Ice Boy amefunguka kuhusu bifu kati ya msanii Jux na model Calisah kwa kusema wawili hao wanafanya 'drama' na hawapo serious.

Kuanzia kushoto kwenye picha ni Ice Boy, Jux na Calisah

Chanzo cha bifu hilo ni kutambiana kwa Jux na Calisah hasa kwenye upande wa mavazi na mionekano yao ambapo rapa Ice Boy anasema hata yeye bifu hilo ameliona zaidi mitandaoni hivyo hawezi kuwajaji.

"Kwa upande wangu mimi nimeona kama ni drama tu sidhani kama ni watu ambao walikuwa serious, niliona wanatafuta attension kwa watu, kila mtu anajua umuhimu wake kwenye sehemu yake, Jux anajua watu wake wanapenda anavyovaa na Calisah naye anajua watu wake wanapenda anavyoonekana" amesema Ice Boy

Kwa sasa Ice Boy ni mmoja wa wasanii wanaotajwa kuongoza kwenye upande wa mitupio na style zake hasa muonekano wake unaofananishwa na marehemu Tupac Shakur.