Jumatatu , 12th Apr , 2021

Staa wa filamu Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amesema akijaaliwa watoto wake basi watu watawaona wakiwa wanaenda shuleni, barabarani, clinic na hata waficha bali atawaacha waishi maisha ya kawaida.

Msanii wa filamu Elizabeth Michael

Aidha kwenye suala la kuwapa uhuru watoto kutumia mitandao ya kijamii Elizabeth Michael amesema ataangalia umri wake na kumpa mipaka kwa sababu ni vitu ambavyo vina athari kubwa kwa mtoto.

"Kiukweli hata mimi inshaallah nikijaaliwa watoto, watu watawaona shuleni, clinic au barabarani yaani sitawaficha ila watawaona kwenye maisha ya kawaida tu, kuna kipindi nilikuwa nafanya tofauti katika malezi ya mdogo wangu ila akili ikaja kubadilika baadae

"Huku mitandaoni tupambane wenyewe tu, lakini kama mtoto atafika umri wa kuamua anataka nini 'its okay' wazazi ku-support ila kwa mipaka fulani maana sio kwamba mitandao ndio chanzo kikuu cha kuleta negative impact kwa mtoto, ila ni moja ya chanzo na kiko 'very tricky' ni kuomba Mungu pia" ameongeza 

Elizabeth Michael ametoa comment hiyo kufuatia stori ambazo zinaendelea mitandaoni kwa sasa kuhusu msanii wa filamu Kajala Masanja na mtoto wake wa kike Paulah.