Jumamosi , 15th Mei , 2021

Ni historia nyingine kwa 'First lady' wa Konde Gang Anjella baada kufikisha watazamaji 'views' Milioni 1 kwa siku moja kwenye mtandao wa YouTube ambapo CEO wake Harmonize amemwambia asivimbe kichwa bali aheshimu kila mtu na kufanya kazi kwa bidii.

Picha ya msanii Anjella na Harmonize

"Najivunia wewe Queen, siku moja views Milioni 1 sio suala dogo unatakiwa umshukuru Mungu na wala isikuvimbishe kichwa jua tu ndio mwanzo wa safari yako, Tanzania imekupitisha na kukupokea, unachotakiwa ni kuendelea kufanya kazi na kumtanguliza Mungu" 

"Heshimu kaka zako na dada zako sio kwa sababu unawazidi namba mkitoa ngoma siku moja basi ikawa chanzo cha kuwavunjia heshima hata kaka yako sipo hivyo siku zote nashukuru kwa ninachokipata kiwe kikubwa au kidogo" ameeleza Harmonize

Kwa sasa msanii Anjella ameachia kazi yake mpya inaitwa 'No body' ambayo ipo namba 2 'on trending' mjini YouTube.