
Happyness Watimanywa - Miss World Tanzania 2014
Katika muda atakaokuwa London, Happyness atajishughulisha pia na baadhi ya mambo ambayo yataitangaza zaidi Tanzania, na yeye binafsi ikiwepo mahojiano na baadhi ya vituo vya kimataifa vya habari.
Happyness amesema kuwa, atamtembelea balozi wa Tanzania nchini humo kwa mualiko maalum, na pia atafanya mahojiano na vyombo vya kimataifa vya habari, ikiwepo BBC Idhaa ya Kiswahili.