Ijumaa , 11th Dec , 2020

Mchekeshaji anayetamba kwa sasa Hakika Ruben amemchana mchekeshaji Anko Zumo kwa kusema jamaa anajisikia sana ndiyo maana hata kwenye vikao vya familia huwa wanamkataa.

Mchekeshaji Hakika Ruben kwenye picha kubwa katikati na Anko Zumo na mwanaye kwenye picha ndogo upande wa kushoto

Hakika Ruben amesema Anko Zumo ni ndugu yake kabisa na anamwita baba mdogo ila kutokana na tabia yake huwa hawazungumzi naye kwenye ukoo wao.

"Mimi na Anko Zumo ni ndugu baba mdogo wangu, alitoka kwetu akaja huku Dar Es Salaam kwa hiyo alitukataa ndiyo maana kuna risk ya ugomvi ni wale ndugu ambao wanajisikia sana hata kuna baadhi ya vikao kwenye ukoo wetu hatuwaitagi kwa sababu wana vurugu na hatuzungumzi nao, tumewanunia kabisa" amesema Hakika Ruben 

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.