Hakeem 5
Akiongea ndani ya eNewz amesema anaweza kuishi akiwa anafanya muziki na hata asipofanya hivyo anaweza akaishi hivyo hawezi kwenda kumuomba Kiba msamaha kwa kuwa yeye hakutaka kufanya kolabo na Kiba ila Kiba ndiye alimuomba wafanye kolabo.
Hata hivyo Hakeem 5 hakusita kumjibu Abby Skills na kumuambia kuwa aache unafiki na aendelee na mambo yake kwani hajui chanzo na angekuwa anataka amani angekaa akawapatanisha kama ndugu na siyo kukaa na kuanza kumkandamiza kwenye vyombo vya habari.