Alhamisi , 12th Mar , 2020

Mrembo na msanii  Haitham Kim, ametangaza na kusema yupo tayari kuolewa na wanaume watatu tofauti, endapo watammudu vizuri kuanzia upendo, kujali,kuridhishwa na kupewa mahitaji yote ambayo mwanamke anatakiwa apatiwe.

Mrembo Haitham Kim

Akieleza sababu ya kutaka kuwa na wanaume watatu, Haitham Kim amesema hawezi kukubali kuumizwa na mwanaume mmoja kwenye mapenzi, wakati wapo wengine ambao wanamuhitaji kuwa naye.

"Inawezekana nikaolewa na wanaume watatu kama watanimudu vizuri, unajua wanawake tunapenda wanaume watuonyeshe upendo, mahaba na kunijali kwahiyo wakitokea wa kufanya yote hayo nipo tayari, pia siwezi kuumia kwa mtu mmoja wakati kuna wengine wananihitaji kwa muda huo" ameeleza Haitham Kim.