Goodluck Gozbert
Akizungumza na EATV & EA Radio Digital kuhusu namna ya muziki wake unavyozungumziwa na watu mbalimbali kwamba hauendani na mahadhi ya kuwa nyimbo za Injili, Goodluck anasema kwake hana cha kusema na huwa anaacha hivyo hivyo.
"Sio kila Mwimbaji anaimba nyimbo za Injili hata kama anaitwa mwimbaji wa nyimbo za Injili, maana ukizungumza nyimbo za dini ni nyimbo zinazohusu dini fulani na nyimbo za Injili ni nyimbo zote zinazo ongelea habari zote ziletazo wokovu," aliongeza.
Goodluck ameendelea kueleza kuwa, kuna waimbaji wanaimba nyimbo za Injili lakini wao wana muabudu Mungu tu na wengine wanamsifu Mungu peke yake hivyo tupo tofauti lakini wote huwa tunaitwa waimbaji wa nyimbo za Injili nayo ni sawa," aliongeza zaidi.
Pia aliongeza mabadiliko ya Teknolojia yamewafanya na wao pia wabadilike lakini Injili ni ile ile na muziki wao pia upo vile vile.