Jumanne , 6th Jan , 2015

Msanii wa muziki GNL Zamba, amepata pigo jingine katika lebo yake ya Baboon Forest baada ya msanii wake wa nguvu kati ya wale wachache waliobakia, Big Tril naye kufungasha virago na kukatisha mkataba na lebo hiyo.

msanii wa muziki wa nchini Uganda GNL Zamba

Kuondoka kwa Big Tril katika lebo hiyo kumeelezwa ni kutokana na shavu alilopata msanii huyu katika lebo maarufu ya kimataifa ambayo itasaidia kuvusha sanaa ya msanii huyu nje ya mipaka ya Bongo.

Kitendo cha Big Trill kuiacha Baboob Forest kinaonesha kuwepo na tatizo katika masuala ya usimamizi wa kazi za wasanii na vilevile uongozi wa GNL Zamba mwenyewe katika lebo hiyo.