Alhamisi , 18th Jun , 2015

Staa wa michano wa nchini Uganda, GNL Zamba ambaye amefanya ziara yake huko Marekani ameeleza kuhamasishwa kwa kiasi kikubwa na mastaa wakubwa nchini humo wanaofanya vizuri katika muziki na filamu, akiwepo Jamie Foxx, Tyrese Gibson na Ice Cube.

Kwa njia ya mtandao GNL amewataja nyota hao kama vivutio vikubwa kwa sanaa yake, akiwa na lengo kubwa la siku moja kuingia katika vinyang'anyiro vya tuzo zenye heshima kubwa kimataifa ikiwepo Grammys na Oscars.

Hatua hii ya GNL pia inalenga kuwahamasisha wanasanaa chipukizi kuwa na ndoto kubwa na kuzifanyia kazi kuelekea mafanikio yao.