
Msanii Gigy Money
Mrembo huyo amefunguka hayo kupitia kipindi cha SalamaNa ambacho kinaruka kila siku ya Alhamisi kuanzia 3:00 usiku ndani ya East Africa TV.
"Kunizoea inabidi uwe na mazoezi ya afya yako ya mwili kwanza, uwe unakula vizuri matunda kama haya hapa, unajua unahitaji kuwa msafi kunishinda mimi ndiyo unizoee au unijue kwasababu nimeamua kuishi kama mjinga ila najijua” amesema Gigy Money.
Aidha msanii huyo ameongeza kuwa kwenye maisha yake ameshawahi kwenda kwa mganga kutokana na kampani ya watu ambao wamemzunguka "Mimi nishaenda kila sehemu nimeenda Msikitini, nimeenda kwa mganga na nimeenda Kanisani, ila nimeshawahi kurogwa kweli na viliniingia na ninajua nilivyojisikia".