Alhamisi , 30th Nov , 2017

Msanii Gigy Money amemtolea povu muigizaji wa filamu wa bongo Rado, ambaye wiki iliyopita alisikika akisema wasanii wa kike wa bongo fleva hawana vigezo vya kuolewa, na kusema kwamba ndoa siku hizi haina dili kwani wanawake wanajioa wenyewe.

Gigy ameyasema hayo alipokuwa akiongea na mwandishi wa East Africa Radio, na kusema kwamba suala la kuolewa miaka ya sasa halina dili sana kwani wanawake wanaoa wenyewe kwa kujilipia mahari, na kumtaka Rado apambane na hali yake kwa kutokuwa na hela ya kuweza kuwapata watoto wazuri.

Msikilize hapa chini