Foby na Hamisa Mobetto
Kupitia eNewz ya EATV, Foby amesema kuwa Hamisa amekuwa ni mbinafsi wa kujijali yeye kuliko wengine ndiyo maana anaongea mambo mengi ambayo hayana msingi.
"Ili uone kuwa Hamisa ni mbinafsi na anajijali yeye kuliko wenzake, nilimtumia wimbo wangu ambao haukutoka rasmi nilitaka yeye ajifunze kuingiza sauti lakini akaniambia mimi mwandishi wa wimbo eti ngoja ausikilize", amesema Foby.
"Kinachoniuma ananiharibia CV yangu ya ukweli, mimi nafahamika ni mtu mkweli. Nilikutana na Mobetto kipindi yupo katika hali ngumu na mambo mengi yalikuwa yanamuandama, hali aliyokuwa nayo kabla hajatoka ni tofauti na aliyokuwa ananionesha baada ya kutoka", ameongeza Foby.
Mtazame zaidi hapa chini akizungumza.
