Alhamisi , 15th Feb , 2018

Rapa Fid Q amepatwa na kigugumizi kwa kushindwa kuweka bayana kama naye anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake mpya anayeishi Tanzania na Uingereza aliyetambulika kwa jina la Karima katika siku za usooni kama ilivyokuwa kwa swahiba wake AY.

Hayo yaliibuka baada ya Fid Q kushindwa kujibu swali aliloulizwa na mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, alilotaka kufahamu kama wana 'plan' zozote za ndoa katika mahusiano yao ndipo Kubanda aliposema hawezi kulitolea majibu suala la ndoa kwa kuwa amezoeleka sana kuzungumza hivyo anamuachia mpenzi wake Karima alitolee ufafanuzi.

"Mimi ninavyoona vitu kama hivyo sio vya kuvikimbilia sana, kuna umuhimu wa kujuana pande zote mbili maana kuna 'good side na bade side too'. Kwa sababu kila mtu anayo ya kwake na ukiangalia mimi natumia muda mwingi nikiwa Tanzania na Uingereza kwa hiyo nataka tui-balance kama tulivyokubalina kwa muda kadhaa japokuwa hatujaweka muda maalumu", amesema mchumba wa Farid Kubanda 'Fid Q' (Karima).

Kwa upande mwingine, Karima amedai wazazi wa pande zote mbili wamefurahia mahusiano yao waliyokuwa nayo hivyo endapo mambo yatakuwa sawa, suala la ndoa halitakuwa na shida.