Alhamisi , 23rd Apr , 2015

Staa wa Muziki Fid Q, ametegua mojawapo ya fumbo kutoka katika video yake ya Bongo Hip Hop kuhusiana na mabinti wawili ambao wamewakilisha vizuri ndani ya kichupa hicho.

msanii wa miondoko ya Hip Hop nchini Fid Q

Rapa huyo ameeleza kuwa mabinti wawili waliotumika katika video hiyo na kuleta tafsiri tofauti, mmoja anawakilisha muziki wa Hip Hop na mwingine akiwa anawakilisha Bongo Flava.

Fid Q ambaye anabeba sifa ya kusuka mistari na kuunda maana katika kila anachokifanya kupitia sanaa yake, amesema akipata nafasi atachambua maana zote zilizojificha katika video hiyo, kubwa likiwa ni kuonesha mvuto wa Bongo Flava dhidi ya ule wa Hip Hop kwa kutumia warembo.