Alhamisi , 27th Sep , 2018

Rapa mkongwe nchini Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q, ameonyesha hali ya kutekwa kimapenzi na mchumba wake anayejulikana kwa jina la Karima, kwa kile alichokionyesha mitandaoni kumuhusisha kwenye sanaa anayofanya.

Fid Q

Hayo yamebainika kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, huku akijaribu kuwauliza mashabiki zake kuwa endapo atatumia picha ya Karima kama 'cover' kwenye albamu yake mpya anayotaraji kuitoa siku za hivi karibuni je wangeipa jina gani jipya albamu hiyo.

"Kama kweli hii inafaa kuwa kava la albumu, unadhani 'title' ipi itafaa?. Mimi nina hisi #GitaaOLOJIA itafaa.. Wewe je!!? #MamaCheusi", ameandika Fid Q.

Kutokana na suala hilo, baadhi ya mashabiki wa Fid Q wamempinga juu ya kitendo hicho cha kutaka kubadilisha jina la albamu huku wengine wakimpongeza kwa anachotaka kukifanya kwa kutaja jina linalofaa.

"Dah kweli ngosha umeshikwa sehemu mbaya, hadi unataka umuweke mama kwenye 'cover' album daah", ameandika kilaki_loishiye.

"Ama kweli mwenye nguvu katekwa hahaha", ameandika nilla23_gt.

"Dah sijaamini kama umeshikwa", ameandika farida lukona.

"kwa muonekano wa pozi la mama hapo na 'guitar' flan + ngoma za huko. Kispaniola "Elegido" 'means chosen one' inafaa.. Kwa sababu ssi ni 'chosen generation' wa kukusikia katika ulimwengu wa technolojia", ameandika nyampa44.

www.eatv.tv ili mtafuta Fid Q kwa njia ya simu kuweza kuzungumza naye juu ya jambo hilo lakini kwa bahati mbaya jitihada hazikuweza kuzaa matunda.

Fid Q ni miongoni mwa wasanii wanaotarajia kuachia albamu aliyoipa jina la 'kitaa olojia' ndani ya mwaka huu.