Jumatatu , 16th Nov , 2015

Msanii Witness amesema kwa sasa yupo tayari kuachia nyimbo yake inayoitwa BUKU JERO pamoja na nyimbo nyingine, baada ya kupona ugonjwa wa uvimbe katika kizazi uliokuwa ukimsumbua kwa takribani miezi minne.

Witness ameyasema hayo alipokuwa akiongea na timu ya Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kuwa tatizo hilo la kiafya limemrudisha nyuma, lakini kwa sasa yuko vizuri na ataendelea kuachia kazi mbali mbali alizozifanya.

“Ni kweli mwaka unaisha na kwa bahati mbaya kuna suala la kiafya lilikuwa limenirudisha nyuma kidogo, na kuna wimbo wangu unaitwa buku jero ambao nilitakiwa niwe nimeufanya by now, lakini niliyvoanza kufanya mazoezi ya dance ikaenda kuibua ugonjwa ambao unaitwa Fibroids, so baada ya hapo nimekaa miezi mitatu kama minne hivi nafanya mpango wa kutibiwa na sasa hivi nimekaa vizuri, kwa hiyo tunaifanya hiyo buku jero wikiendi hii, alisema Witness.

Witness amesema pamoja na kufanya video ya buku jero pia anatarajia kuachia wimbo mpya ambao aliurekodi siku yake ya kuzaliwa.

“Then kitu kingine kuna ngoma nyingine mbali na buku jero, pia iko tayari ambayo nimeirekodi usiku wa kuamkia birthday yangu ambayo ilikuwa ni tarehe 15 jana, na pia projects nyingine zinakuja tuombe uzima”, alisema Witness.