Jumapili , 8th Nov , 2015

Diwani wa kata ya Kilungule Said Fella au Mkubwa Fella amesema kuwa hivi sasa ameanza kuweka nguvu kazi katika kuijenga kata hiyo ambayo hivi sasa inahitaji uboreshaji mbalimbali ikiwemo pia miundombinu.

Diwani wa kata ya Kirungule ambaye pia ni msanii wa muziki Said Fella

Meneja huyo ambaye pia ni mmiliki wa kituo cha Wanawe amesema ana imani kuchaguliwa na wanachi wa kata hiyo huku akiweka wazi kuwa changamoto za uboreshaji kata hiyo ni haswa katika sekta za barabara, visima, zahanati, mashule na mengineyo mengi.

Akiwa ni msanii na mmiliki wa kituo chake cha Mkubwa na Wanawe ambacho kinaendelea kuinua wasanii chipukizi wa jinsia zote, amesema kuwa japokuwa ameingia katika udiwani, nafasi yake kama meneja wa kituo hicho bado ipo na hivi sasa anazidi kutoa kipaumbele kwa vijana nchini katika kutimiza ndoto zao.