Jumamosi , 23rd Mei , 2015

Msimamizi wa kazi za wasanii na muasisi wa kundi la Mkubwa na Wanawe, Said Fella amesema kuwa viongozi wa serikali wangeweza kuichukulia Bongo Fleva kama moja ya sekta rasmi inayosaidia kupunguza ugumu wa maisha kwa vijana, wangeipatia heshima zaidi.

Said Fella

Fella amesema kuwa, Viongozi hawa wanatakiwa kukaa tena na kuitazama Bongo Fleva kwa undani na kuitambua vizuri hatua ambayo itaipatia heshima sekta hiyo ambayo waasisi wake, akiwataja wakina Salehe Jabir na Proffesa Jay walifanya kazi kubwa kuipatia maana na kuifanya ajira ambayo imeweza kubadilisha maisha ya vijana wengi kwa sasa.

Fella ambaye kwa mujibu wake ameingia katika sekta hii mwaka 1999 na kukuta tayari inaanza kuingia katika mstari, ametoa wito kwa sekta hiyo kupatiwa maana zaidi ikiwa ndani yake na ina vitengo mbalimbali ambavyo kundi kubwa la vijana waliopo mtaani wanaweza kujishughulisha nazo na kujipatia vipato na kupunguza ugumu wa maisha.