![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2019/12/07/BOSCO.jpg?itok=LGemHin_×tamp=1575723505)
Picha ya marehemu Seth Bosco
EATV & EA Radio Digital imempata msemaji wa chama cha waigizaji aitwaye Masoud Kaftan, ambaye ameeleza chanzo cha kifo chake na taarifa kamili kuhusu siku ya mazishi ya Seth Bosco.
"Marehemu alikuwa anasumbuliwa na uvimbe kwenye uti wa mgongo, kabla ya kufariki alienda hospitali ya Muhimbili kisha akarudi nyumbani, ila kuanzia mida ya saa 12:00 jioni akaanza kupata baridi kali, kujisikia vibaya ilivyofika usiku saa 4:00 au 5:00 akaanza kubadilika na ilivyofika saa 6:00 usiku akakata roho" ameeleza msemaji wa waigizaji Masoud Kaftan.
"Msiba upo nyumbani kwa Mama wa marehemu Kimara Temboni, sasa hivi tupo katika mipangilio ya vikao, lengo tulikuwa tunaomba tukamzikie katika makaburi ya Kinondoni siku ya Jumatatu Disemba 9, kuanzia mida ya saa 8:00 mchana hadi saa 10:00 jioni, tuwe tumeshamstiri" ameongeza.