
Idris Elba
Idris ambaye ana umri wa miaka 43 sasa, ameeleza kuwa tukio lenyewe lilikuwa ni juu ya maporomoko ya maji ambapo aliteleza futi sita chini kabla kugota na kuokolewa na moja ya walinzi waliokuwepo eneo la tukio.
Filamu ya Beasts Of No Nation inabeba kisa cha mvulana ambaye alilazimishwa kuwa mwanajeshi huko Afrika Magharibi, ikiwa ni moja ya kazi ambayo ilikuwa na changamoto nyingi kwa star huyo na timu yake kuifanya, ikiwepo muongozaji wake kuumwa Malaria kali wakati wa upigaji picha za kazi yenyewe.