Jumatatu , 5th Sep , 2016

Msanii Eddy Kenzo wa Uganda amezizungumzia tuzo kubwa zilizoanzishwa Afrika Mashariki za muziki na filamu (EATV AWARDS), na kusema kuwa ni jambo la heri kwa wasanii wa Afrika Mashariki.

Eddy Kenzo

Eddy Kenzo ambaye ni moja ya wasanii wanaofanya vizuri zaidi nchini Uganda, amepiga stori na mwandishi wa EATV na kusema kuwa wao kama wasanii wamekuwa wakizikosa tuzo kama hizo kwa muda mrefu, lakini sasa ni fursa kwao wasanii wa Afrika Mashariki, kuweza kufanya kazi bora zitakazowafikisha mbali pia.

"Ni kitu kizuri sana, ni mawazo mazuri , nafikiri tumekuwa tukikosa hii kwa miaka mingi mingi sana, nafikiri itakwenda kuweka umakini kwa jamii na itaenda kuboresha uburudishaji wetu miongoni mwetu, kwa sababu ni kitu kikubwa sana, na itaenda ku'boost' mziki wa Afrika Mashariki, kwa sababu mwisho wa siku ni mashindano, na unatakiwa uhakikishe unafanya kazi kwa bidii kuhakikisha ni nzuri, kufanya kazi ya mashindano kila mmoja atajikuta yuko juu ".

Eddy Kenzo amekuwa msanii wa pili kutoka nchini Uganda kuzizungumzia #EATVAwards, baada ya Bebe Cool kusema kuwa tuzo hizo zitawaunganisha tena wasanii wa Afrika Mashariki.

Tags: