Ijumaa , 28th Feb , 2020

Mchekeshaji Ebitoke ametangaza nia ya kugombania taji la Miss Tanzania mwaka 2020,kwa Kanda ya Ziwa.

Mchekeshaji Ebitoke akiwa ameshika fomu ya kuwania taji la Miss Tanzania 2020

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mchekeshaji huyo ameweka taarifa ya kugombania urembo huo baada ya kupost fomu ambayo ina picha yake ikionesha yupo tayari kushindania taji hilo.

"Ahsanteni sana mashabiki wangu kwa support mnayoendelea kunipa, napenda kuwajulisha rasmi tayari nimeshajaza fomu ya kushiriki Miss Tanzania kanda ya Ziwa 2020, nikiwakilisha Mkoa wangu wa Kagera na nimei-submit kwa wahusika, ni imani yangu kwamba nitafika mbali na nahitaji support yenu" ameandika Ebitoke

Taji hilo la urembo kwa sasa analishikilia Miss Tanzania 2019, Sylivia Sebastian.