Jumanne , 13th Dec , 2016

Msanii wa filamu nchini Tanzania ambaye alikuwa kwenye kinyang'anyiro cha muigizaji bora wa kike katika tuzo za muziki na filamu za EATV, Khadija Ally ameibuka na kutoa shukrani zake kwa EATV, wadhamini wa tuzo hizo pamoja na watu waliompigia kura.

Khadija Ally

Khadija ambaye aliingia kwenye tuzo hizo kupitia movie yake ya 3Days, ametoa shukrani kupitia ujumbe mfupi alioutuma kwa wadau wote, na kusema kuwa tuzo hizo zimemuweka mahala pazuri katika tasnia ya filamu nchini licha ya kutoshinda katika kipengele hicho.

Pia Khadija hakusita kuwapongeza wasanii wenzake aliokuwa nao katika kipengele hicho hasa mshindi ambaye ni Chuchu Hansy, huku akisema kuwa wasanii wote walikuwa bora, lakini ni lazima mshindi awe mmoja, hivyo inategemeana na bahati ya mtu, na kwamba anakubaliana na maamuzi yaliyotokea.

Khadija amesema "Kwanza kabisa nashukuru Eatv, East Africa Radio, Vodacom, Cocacola na Barclays bank kwa kuandaa Eatv Awards mie nasema asanteni na asiyekubali kushindwa si mshindani pia nawapongeza wote waliopata tunzo, na ninaamini wote tulikua bora ila kupata tunzo ni bahati tu". 

Baadhi ya washiriki wakifuatilia tukio la utoaji tuzo katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam

Tags: