Jumamosi , 19th Sep , 2015

Msanii Dully Sykes ambaye wiki hii ameachia kimya kimya rekodi yake mpya inayokwenda kwa jina 'Kwani wewe ni Nani, amefafanua kuwa hiyo si kazi rasmi kutoka kwake, akiwa ameamua kuiachia mitandaoni pekee kwaajili ya kuwapatia ladha tu mashabiki wake.

Dully Sykes

Dully Sykes amesema kuwa, rekodi hiyo vilevile si kwaajili ya kupima upepo endapo itafanya vizuri ama itabuma kama ambavyo baadhi ya wasanii wamekuwa wakifanya, hii ikiwa ni matayarisho tu ya ujio wake rasmi.