Jumamosi , 2nd Jan , 2016

Band ya Muziki wa Dansi toka nchini inayoongozwa na Mkongwe Prince Muumini Mwinjuma ya Double M Plus wako mbioni kurejea nchini kuanza ziara za kimuziki ikiwa ni pamoja na kurekodi nyimbo zao baada ya kuweka kambi nchi msumbiji kwa muda mrefu.

Waimbaji wa Band ya Double M Plus wakiwa katika pozi tofauti

Akiongea na Enews Prince Muumini amesema tayari wameshakamilisha nyimbo nane ambazo zitakua katika album yao ambazo wamezipiga katika mitindo tofauti tofauti ili kuwapa ladha mashabiki wa aina zote za muziki wa live nchi.

Prince amesema licha ya band hiyo kuundwa na wanamuziki wakali kama Salehe Kupaza, Dogo rama na wengine wenye vipaji kwa sasa wako katika mandalizi ya kurejea bongo kwa ajili ya utambulisho wa band ambayo amesema italeta mapinduzi nchini.