Jumanne , 11th Mei , 2021

Ukurasa rasmi wa marehemu DMX umetoa taarifa za ujio wa album yake ‘Exodus’ kuwa itaachiwa Mei 28 mwaka huu chini ya Def Jam Records.

Msanii DMX

Hii itakuwa album ya kwanza ya DMX tangu afariki mapema Aprili mwaka huu na ya kwanza chini ya Def Jam tangu 'Grand Champ' ya mwaka 2003.

Exodus imetayarishwa na Swizz Beatz ambaye ndiye mtayarishaji mkuu.