
Kushoto ni director Joowzey na kulia ni director Eddy
Wakiongea kwa nyakati tofauti, 'Director' wawili Joowzey pamoja na Eddy wamejikuta wakipishana kauli baada ya kila mmoja kuwa na mtatzamo tofauti inayoashiria au kuelezea kwa nini video nyingi zimekuwa zikijirudia haswa za mwaka 2018.
Joowzey amefunguka kwamba video zinakuja kuonekana zinafanana kwa sababu waongozaji wengi wa video wamekuwa wakienda na fasheni kulingana na wakati na kujikuta wanatumia idea za kufanana huku Eddy akikiri kuwa ni tatizo lakini linatokana na ukosefu wa maeneo ya kufanyia video.
"Hakuna ukweli wowote kuhusiana na fasheni kwa uandaaji wa video zetu bongo, kitu pekee ambacho kinatuangusha ni kutokana na ukosefu wa 'location' hali inayopelekea hata ukirekodi video moja mwezako akikupigia simu umuambie 'location' ilipo unakuwa huna budi kumuambia ni wapi kwa kuwa hakuna namna 'location' ni chache," aliongea Eddy.