Jumatano , 28th Oct , 2015

Wasani kutoka hapa nyumbani Tanzania watakaopanda jukwaa moja na msanii mkubwa wa kimataifa toka nchini Nigeria WIZKID pale viwanja vya Leaders Club siku ya jumamosi hii Oktoba 31, wametajwa rasmi leo

Wasanii hao ni pamoja na Diamond Platnumz, kwa upande wa HIP HOP ataiwakilisha vyema Fid Q na bila kumsahau mkali wa masauti Christian Bella.

Kumbuka viingilio vya onesho hili kubwa la burudani siku ya jumamosi ni shilingi elfu 20,000 kwa viti vya kawaida na viti maalum ni shilingi laki 100,000
Baada ya kumjua Rais wetu mpya, tunaenda kula burudani pamoja pale Leaders Club toka kwa mkali wa mambo hizi WIZKID toka Nigeria akipewa shavu na wakali hao toka Tanzania