Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City na kupambwa na burudani za kutosha pamoja na washereheshaji waliokonga nyoyo za mashabiki, wasanii waliong'ara ni pamoja na Diamond Platinumz aliyenyakuwa tuzo Saba, Lady Jaydee, Farid Kubanda Fid Q , Isha Mashauzi, Mzee Yusuf pamoja, na Niki wa Pili waliotwaa tuzo mbili kila mmoja.
Wasanii wengine wa Muziki waliong'ara na kuibuka na tuzo ni pamoja na Young Killer, Chibwa, Luiza Mbutu, Josee Mara, Rapa Ferguson, Vanessa Mdee, Ney wa Mitego, Dabo pamoja na Vikundi kama vile Bendi ya Mashujaa , Jahazi Modern Taarab, ambapo Man water nae aling'ara katika utayarishaji wa Muziki.
Hafla hii ya Tuzo za Muziki za Kilimanjaro ilipambwa na burudani kali kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongofleva akiwepo Vanessa, Ommy Dimpoz, Weusi, Fredy Zaganda na wengineo.