Alhamisi , 17th Apr , 2014

Msanii wa muziki Diamond Platinumz, amepiga hatua nyingine kubwa kwa muziki wake nje ya mipaka ya Tanzania, baada ya kuingia katika kinyanganyiro cha tuzo za muziki zinazoandaliwa na kituo cha kimataifa cha Televisheni kupitia tawi lake Afrika.

Diamond

Diamond anaingia katika kinyanganyiro hiki kupitia wimbo wake wa My Number One Remix katika kipengele cha kolabo bora, na vile vile anatokea katika kipengele cha msanii bora wa kiume huku akipambanishwa na wasanii wengine wakubwa Afrika ikiwa ni hatua kubwa kabisa kwa msanii huyu kutoka hapa Tanzania kupeperusha bendera yam Tanzania katika ngazi ya kimataifa.

Zoezi la kuwapigia kura wasanii wote wanaowania tuzo hizi tayari limeanza kwa njia ya mtandao mpaka tarehe 4 mwezi Juni, ambapo sherehe kubwa za kugawa tuzo kwa washindi zitafanyika huko Afrika Kusini tarehe 7 mwezi Juni mwaka huu.