Jumatatu , 30th Jun , 2014

Msanii Diamond Platnumz, amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa mapambano ndio yanaanza sasa katika safari yake ya muziki, baada ya kumalizika kwa tuzo za BET alizokuwa akiwania katika kipengele cha msanii bora wa kimataifa kutoka Afrika.

Msanii Diamond wa nchini Tanzania

Kufuatia tukio hili la msanii Davido kutwaa tuzo hiyo, mashabiki na wadau mbalimbali wa muziki hasa kutoka hapa Tanzania wametoa maoni tofauti kwa njia ya mtandao huku wengi wakimpongeza Diamond kwa hatua aliyofikia kwa kuwa moja ya wasanii wanaowania tuzo ya BET.

Kutoka katika tuzo hizi, Lupita Nyong'o ameweza kung'ara pia akiibuka kama mwigizaji bora wa kike na pia filamu ya 12 Years a Slave aliyoshiriki kuibuka kama Filamu Bora.

Kwa upande wa muziki kimataifa, wasanii Nicki Minaj, Beyonce, Drake likiwepo kundi la Cash Money, wameweza kung'ara zaidi katika tuzo hizi kwa kuibuka na tuzo na pia kwa maonyesho ya aina yake.