
Msanii wa miondoko ya bongo fleva nchini, Darasa
Darasa amejitaja kama rapa ambaye mashabiki wake walimuamini ndani ya kipindi kifupi na yeye kugundua kuwa kuna sehemu hakuwatendea haki, na hivyo rekodi yake mpya ya Tunaishi inakuwa ni kazi ambayo anaamini inatoa majibu na kumrudisha katika nafasi yake kimuziki.
