Alhamisi , 16th Jul , 2015

Akiwa ni mmoja wa madiva wakali wa muziki wa kizazi kipya nchini msanii Pam Daffa atoa ya moyoni kuhusiana na wasanii Mr Blue na Juma Nature kwa kile anachosema kuwa anawazimia wakali hao.

msanii wa miondoko ya bongofleva nchini Pam Daffa

Pam Daffa ameongea na eNewz kuwa amekuwa akifuatilia kazi zao kwa muda mrefu huku akijiandaa kujumuika na wasanii wakongwe katika gemu akiwemo Feruz, gangwe Mob, katika tamasha kubwa la muziki huko Changombe jijini Dar es Salaam akiweka wazi kuwa atafanya kazi kukaribu na wakali hao.