Ijumaa , 10th Jul , 2015

Msanii wa muziki wa bongofleva Barakah Da Prince ambaye aliyetwaa tuzo ya muziki ya Kili mUsic Awards kama msanii anayechipukia wa mwaka huu amesema kuwa katika madiva wakali anaowazimia katika muziki ni Ruby pekee.

wasanii wa muziki wa bongofleva Barakah na Ruby

Akiongea na enewz Baraka amesema alivutiwa sana na mwanadada huyo na walikutana studio kwa mara ya kwanza ndipo baadae alianza kufanya nae matayarisho ya kurekodi wimbo mpya 'Nivumilie' aliomshirikisha diva huyo ambao tayari ulikuwa umeandikwa na prodyuza Lolipop na hapa mkali huyo anafunguka zaidi.

Aidha mkali huyo anayetamba na kibao cha 'Siachani Nawe' hakuacha kutoa sifa na pongezi kwa wasanii wengine wa kike nchini na pia kuhusu mpango wa kufanya video ya wimbo huo mpya 'Nivumilie'.