Alhamisi , 1st Dec , 2022

Boss wa Kondegang Music Worldwide Harmonize ametangaza kuchaji Tsh Milioni 100 kwa wasanii watakaotaka kufanya naye Collabo huku sharti lake ngoma iwe kali tu.

Picha ya msanii Harmonize

"Naanza kuchaji Tsh Milioni 100 kwa collaboration sharti ngima iwe kali. I cant wait kumchaji mtu fulani Milioni 500" ameandika Harmonize 

Kwa mwaka huu 2022 tayari Harmonize ameshirikishwa kwenye ngoma kadhaa kama naogopa ya Marioo, follow me ya Aslay,  furaha ya Iyani kutoka Kenya, na champion remix ya Kontawa.