Alhamisi , 26th Jun , 2014

Cindy Sanyu, mwanamama anayefanya poa kupitia muziki nchini Uganda, yupo katika vita ya kisheria na Mario Brunette aliyekuwa mpenzi na baba mtoto wake, katika mahakama huko Nakawa, wakigombea haki ya malezi ya mtoto wao baada ya kutengana.

Kwa mujibu wa taarifa, Cindy na Mario baada ya kutengana walikubaliana kushirikiana kulea mtoto wao, lakini kadiri muda ulivyokuwa unasogea, Mario akaanza kukomaa kuwa ndiye mlezi anayekaa na mtoto huyu muda wote, kitu ambacho Cindy hakubaliani nacho.

Kwa sasa bado maamuzi ya mahakama kuhusiana na sakata hili yanangojewa, huku ikiwa inafahamika kuwa tayari Cindy amekwishafungua ukurasa mpya wa mapenzi kwa kuanza kutoka na mfanyabiashara Ken Muyiisa.