CHUCHU HANS
Chuchu amesema tamthilia hiyo itahusisha wakali kibao wa zamani na wa sasa akiwemo yeye mwenyewe na wengine kama Nyamayao, Thea, Senga na wengine kibao.
Kwa kiasi kikubwa vile vichwa vingi vya kundi la Kaole vitahusika. Pia Chuchu amesema anaamini vichwa vilivyohusika vitatoa burudani ya uhakika kwa wapenzi wa tamthilia za bongo.
Tamthilia hii itaonesha hali halisi ya usaliti wa kimapenzi katika jamii zetu ikiwa na lengo la kuelimisha zaidi.
Zaidi Chuchu alidokeza kuwa tamthilia hiyo imeandaliwa kisasa zaidi na itakuwa na ubora wa juu kuliko tamthilia nyingi za Bongo.








