Jumatano , 21st Dec , 2016

Msanii wa bendi nchini au wengi wanapenda kumuita mzee wa masauti Christian Bella amefanikiwa kufungua studio yake binafsi inayokwenda kwa jina la Kingdom.

Christian Bella

 

Akizungumzia na eNewz amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na maproducer tofauti tofauti nchini na mpaka sasa hivi yuko tayari kufanya kazi na producer yeyote

“Mimi siyo kama sitafanya kazi na producer wengine bali namaanisha kuwa nitafanya kazi na producer yeyote ninayemtaka na lakini katika studio yangu mwenyewe ni muda mrefu sana nilikuwa natamani kuwa na studio yangu kwa sababu kuna muda mwingine ulikuwa unapeleka nyimbo kwa producer inakaa hata miezi mitatu bila kutoka lakini sasa hivi nimerahisisha na kama nikihitaji "touch" za Man Water au Nahreel au producer yeyote au hata kama ana idea nitamuita na anakaribishwa hapa tufanye kazi”

Christian Bella ni kati ya wasanii wa bendi nchini ambao wanafanya vizuri sana katika  muziki huo, na ndiye msanii wa band anayelipwa hela nyingi katika show zake kwa sasa