Ijumaa , 22nd Jul , 2016

Mkali wa HIP HOP Bongo, Chidi Benz asema ataendelea kuwa mfalme sababu hakuna kama yeye Bongo.

Akiongea na eNewz Chidi alisema, "Kuna wakati nilipotea na nilikuwa dunia nyingine kabisa, lakini nimerudi na sasa kila mtu amefurahi".

Aliongeza kuwa, "hata wasanii wote, nikiwa nao na hata nikiwa mbali nao wanatambua kuwa mimi ni mfalme".

Kuhusiana na anafanyaje kazi na WCB, Je wamemsainisha kama msanii wao? Na je hii inamaanisha utakuwa ndio mwisho wa
LA FAMILIA? Chidi alisema "WCB ni wadogo zangu tu, na ninafanya nao kazi kupush tu mambo mawili matatu, lakini haimaanishi kuwa ndio nimeiacha La Familia, Ile familia yangu".

Lakini alipoulizwa zaidi kama yeye amesainishwa kabisa kama msanii wa WCB Chidi alisema "Mbona hili unaliulizia sana? I hate it man".

Tags: